Jana Ukraine iliweka historia mpya katika uwezo wake wa kijeshi baada ya kufanikiwa kufanya shambulizi kubwa ndani kabisa ya Urusi.
Ukraine ilishambulia ndege za kivita za Urusi zilizo umbali wa kilometa 4300 yaani ni sawa na umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Afrika Kusini.
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa Ukraine, Vasyl Malyuk ameeleza jinsi ilivyokuwa vigumu kufanya shambulizi hilo lililofanyiwa utafiti kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu kabla ya kutekelezwa huku likisimamiwa na Rais Volodomyr Zelensky yeye mwenyewe.
Shambulizi hilo lilifanikiwa kuharibu ndege 40 za kivita za Urusi zilizokuwa katika Uwanja wa ndege wa kijeshi ndani kabisa ya Urusi ili kuzificha dhidi ya mashambulizi ya Ukraine ambayo mara nyingi yaligusa mikoa ya mpakani mwa Urusi na Ukraine.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED