CCM yawaahidi wananchi Hai mambo 10

By Gwamaka Alipipi , Nipashe
Published at 12:17 PM Sep 13 2025
CCM yawaahidi wananchi Hai mambo 10
PICHA: GWAMAKA ALIPIPI
CCM yawaahidi wananchi Hai mambo 10

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa ahadi kwa wananchi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mojawapo ni kumaliza tatizo la ukosefu wa maji.

Mgombea Mwenza wa Urais wa chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel  Nchimbi alitoa ahadi hiyo leo Septemba 13 alipofanya mkutano mdogo wa kampeni wilayani hapa. Dk.Nchimbi alisema miaka mitano ijayo CCM imejizatiti kuleta mabadiliko zaidi wilayani Hai.

"Tutamaliza tatizo la maji. Suala la kuleta gari la kuchimba visima siyo la kusubiri, hilo limeisha. Hilo suala tutalichukulia hatua haraka na halina mjadala. Tunawaka wananchi wa Hai muondokane na tatizo la ukosefu wa maji," alisema Dk. Nchimbi.

Alisema pia CCM itajielekeza katiia kuboresha barabara kwa kiwango cha lami na changarawe pamoja na kupeleka umeme katika kata zote wilayani hapa.Balozi Dk. Nchimbi pia alisema kutajengwa kongani ya viwanda wilayani Hai kwa sababu wakazi wake ni wakulima na wafugaji.

Alisema miaka mitano ijayo CCM kimedhamiria kwenda mchaka mchaka katika kuwaletea maendeleo wananchi.Vilevile alisema serikali itaendelwa kutoa mbegu za ruzuku, kugharamia maofisa ugani, ukarabati wa majosho pamoja na mabwawa ya mifugo. Naye Mbunge mteule wa Hai, Saashisha Mafue alisema CCM wilayani Hai imejipanga kuhakisha Mgombea Urais anaibuka mshindi kwa kupata kura za kishindo.