Salum Mwalimu: Nikiingia Ikulu, nitavunja bodi zote za mazao na za wakulima maana hazifayi kazi yake

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 06:28 PM Sep 13 2025
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu
PICHA: ELIZABETH ZAYA
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), Salum Mwalimu

Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), amesema akiingia madarakani atavunja bodi zote zinazosimamia bidhaa za wakulima kwa sababu hazina msaada kwa Wakulima.

Amesema nchi hii ina watu aliowaita 'wahuni' wachache lakini upo uwezekano mkubwa wa kuinyoosha.Amesema bodi zote zinazoundwa, kwa ajili ya kusaidia wakulima hazifanyi kazi hiyo isipokuwa zipo kunufaisha watu binafsi na kwamba hayuko tayari kuendelea kuwa nazo.

Amesema akingia Ikulu, ataunda chombo kimoja kitakachofanya kazi hiyo ya kusaidia masilahi ya bidhaa na wakulima kwa ujumla.Amesema hayo leo Magu mkoa wa Mwanza wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni ikiwa ni kwa siku ya kwanza ya kampeni kwenye mkoa huo.