Ruvuma yaja na mpango wa kukuza utalii na uwekezaji Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na taasisi ya Ruvuma Picnic and Tourism umeandaa mpango wa kukuza vivutio vya utalii na uwekezaji unaojumuisha maonesho ya utalii yatakayoambatana na matukio yanayolenga kutangaza na kukuza Utalii Mkoani Ruvuma .
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed akizungumza na waandishi wa habari na wananchi kwenye uwanja wa Stendi Kuu ya zamani mjini Songea
"Malengo mahususi ya mpango huu ni kukuza utalii wa kiutamaduni, kihistoria na kiekolojia katika maeneo ya Ruvuma kama vile mapango ya kihistoria, kumbukumbu ya vita vya majimaji, vyanzo vya maporomoko ya maji na maeneo mengine kadha wa kadha."
Sanjari na hayo ametoa wito kwa wananchi na wadau wa utalii kuwa mabalozi wa kutangaza fursa zilizopo ndani na nje ya Ruvuma huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kuyakaribisha mabadiliko chanya na kushiriki kikamilifu katika kuinua uchumi wa Mkoa.
Kwa upande wake Muundaji Mkuu wa Taasisi ya Ruvuma Picnic wamehimiza wakazi wa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kuona umuhimu wa kujitokeza kuutangaza utalii katika fukwe za ziwa nyasa, kwenye Zoo ya wanyama iliyopo katika ya manispaa ya Songea na msitu wa asili mwambesi wilayani Tunduru.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED