Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kinatarajia kuwapokea na kuwateua wajumbe wapya kushika nafasi tatu za juu katika uongozi wa kitaifa wa chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya Chama hicho ni kwamba nafasi zitakazojazwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, Katibu Mkuu, na Naibu Makamu Mkuu wa chama.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa CHAUMMA kuimarisha safu ya uongozi, kuongeza ufanisi wa kiuendeshaji na kujipanga kuelekea chaguzi zijazo. Viongozi wapya wanatarajiwa kutangazwa rasmi katika kikao cha juu cha chama kinachofanyika Mei 19,2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED