Wachimbaji 6 wafariki dunia, 11 majeruhi mgodini

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 05:40 PM May 19 2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akitoa taarifa ya vifo vya wachimbaji sita ambao wamefariki katika mgodi wa Mwakitolyo wilayani Shinyanga huku 11 wakijeruhiwa baada ya mgodi huo kuanguka.
Picha: Marco Maduhu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, akitoa taarifa ya vifo vya wachimbaji sita ambao wamefariki katika mgodi wa Mwakitolyo wilayani Shinyanga huku 11 wakijeruhiwa baada ya mgodi huo kuanguka.

WACHIMBAJI sita wa dhahabu katika mgodi wa Mwakitolyo, namba nane wilayani Shinyanga, wamefariki dunia, huku 11 wakijeruhiwa baada ya kuangukiwa na mgodi huo.

Ajali hiyo imetokea mwishoni mwa wiki, majira ya saa 5:00 asubuhi, wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli za utafutaji  wa madini ya dhahabu.

Eneo amablo wachimbaji 6 wamefariki duni, 11 majeruhi mgodini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, juzi, alifika eneo la tukio na kutoa taarifa kwamba, katika ajali hiyo wachimbaji sita wamethibitika kufariki dunia, huku 11 wakijeruhiwa na wanaendelea na matibabu.“Kwa niaba ya serikali natoa taarifa kwamba imethibitika nwatu sita wamepoteza maisha na wengine 11 wamejeruhiwa na kati yao, mmoja ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata matibabu na wengine 10 wanaendelea kupokea huduma hospitalini,” amesema Macha.
Eneo la tukio ambako wachimbaji 6 wamefariki duni, 11 majeruhi mgodini
Amesema, serikali imeshaanza kuchunguza tukio hilo kwa kina, ili kubaini chanzo chake na kwamba wataweka mikakati madhubuti ya kuimarisha usalama kwenye migodi yote midogo, hasa katika machimbo hayo ya Mwakitolyo.

Nao baadhi ya wachimbaji katika mgodi huo, wamesema kwamba walishitukia tu mgodi ukishuka na kuwafunika wenzao ambao walikuwa chini ya ardhi wakiendelea na uchimbaji, huku wakiishukuru serikali kwa kufika haraka eneo la tukio na kufanya uokoaji.