Serikali yashirikiana na wadau kuinua wazee

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 05:30 PM May 19 2025
Wazee
Picha: AI
Wazee

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau, imeanzisha vikundi 395 vya Uzalishaji Mali vya Wazee, huku wazee 10,926 kati yao wanaume ni 5,333 na wanawake 5,593 wamenufaika na miradi mbalimbali, ikiwamo kuwezeshwa katika shughuli ndogo za kilimo cha mboga, kuwa na vitalu vya miche ya matunda, ufugaji wa nyuki, mbuzi, ng’ombe na kuku.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis, amesema hayo leo Mei 19, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamori, alihoji kwa namna gani serikali inatekeleza takwa la Sera ya uUshirikishwaji wa Wazee katika shughuli za uzalishaji mali.

“Niendelee kutoa wito kwa wazee kutumia mazingira yao kufanya shughuli ndogo ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili. Aidha, nasisitiza jamii kuendelea kuunga mkono juhudi na shughuli zinazofanywa na wazee katika jamii zetu, ili kuimarisha ustawi wao,” amesema