Lissu afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 10:05 AM May 19 2025
Lissu afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali
Picha: Imani Nathaniel
Lissu afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

Hatimaye, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo saa 2:52 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza.

Lissu amefikishwa mahakamani kufuatia agizo lililotolewa na mahakama hiyo Mei 6, 2025, ikielekeza kwamba mshtakiwa huyo aletwe mahakamani leo na wananchi waruhusiwe kuingia ukumbini kusikiliza kesi hiyo.

Lissu anakabiliwa na kesi ya tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni. Inadaiwa kuwa mnamo Aprili 3, 2025, jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kupotosha umma, alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube. Taarifa hizo zilieleza kwamba "Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana, wagombea wa Chadema walienguliwa kwa maelekezo ya Rais."

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mahakamani hapo huku kukiwa na ulinzi mkali na umati wa wananchi waliojitokeza kufuatilia mwenendo wa shauri hilo.