MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) John Heche amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anasogeza uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais mbele ili kupisha marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Heche amesema hayo leo mkoani Morogoro wakati CHADEMA ilipofanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi K,ndege Manispaa ya Morogoro. Anasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina maeneo mengi ambayo yanaketa mkanganyiko ambazo zikifqhyiwa marekebisho nchi itapata viongozi sahihi watakaosaidia wananchi kuondokana na umaskini waliokuwa nao licha ya kwamba nchi yao ni tajiri.
Anasema pamoja na ukubwa wa Tanzania lakini nchi ina kila sababu ya wananchi wake kuitwa tajiri kutokana na mali zilizopo ikiwemo madini ya aina mbalimbali, makaa ya mawe, chuma na mchanga wa kusafishia ambavyo havisimamiwi wala kutumiwa vyema kutokana na usimamizi mbovu uliopo. Anasema CHADEMA ikipata nafasi ya kuongoza nchi baada ya katiba kurekebishwa mzee wa miaka 60 anapata bima ya maisha huku kukiwa na bima ya afya kwa wote.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema mfumo wa bila mabadiliko hawawezi kuingia kwejye uchaguzi hawawezi kuubadilisha hadi serikali iliyopo madarakani ibadilishe vifungu vya sheria ikiwemo sheria inayosema matokeo ya uchaguzi hayawezi kujadiliwa hata mahakamani na mambo ambayo waliyapinga kwa mwaka mzima kwa vikao na Rais wakati wa vikao vya maridhiano bila mafanikio.
Anasema hayo yakibadilishwa yatasaidia hata kuondoa wizi wakati wa uchaguzi uliosababisha japo mwaka 2020 kufanyiwa hujuma kwenye uchaguzi.Hata hivyo Mnyika anasema Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu sio gaidi bali kumuweka ndani na kumpandisha mahakami ni kutaka kupora ihuru wake wa kueleza mambo ya kweli ambayo hata hivyo hawataacha kuyasema.
Mwenyekiti wa baraza Wazee CHADEMA Taifa Suzan Lyimo amewataka wanachadema kushikamana kwa kuhakikisha mabadiliko kwanza yanatokea ili kuepuka usio na haki ambao tayari umeshanza kujitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED