Dk. Kikwete ahitimisha ziara yake Burkina Faso akutana na Rais Ibrahim Traoré

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:57 PM Apr 17 2025


Dk. Kikwete ahitimisha ziara yake Burkina Faso akutana na Rais Ibrahim Traoré
Picha: Mpigapicha Wetu
Dk. Kikwete ahitimisha ziara yake Burkina Faso akutana na Rais Ibrahim Traoré

Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amehitimisha ziara yake nchini Burkina Faso kwa kufanya mazungumzo rasmi na Rais wa nchi hiyo, Kapteni Ibrahim Traoré.

Mkutano huo umefanyika leo, Aprili 17, 2025, katika Jiji la Ouagadougou, na umehudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka serikali za Tanzania na Burkina Faso.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Kikwete alitoa shukrani kwa mwenyeji wake kwa kumpa nafasi ya kuwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Samia, akisema:

1

 "Rais wangu amenituma nije kuwasilisha Ujumbe Maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na leo umeupokea rasmi." — Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.


Aidha, Dk. Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan akisisitiza dhamira ya Tanzania katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika. 

Alisisitiza umuhimu wa kubadilishana uzoefu, ujuzi na rasilimali ili kuhakikisha bara la Afrika linajitegemea na kuwanufaisha wananchi wake kiuchumi na kijamii.

2

Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kuimarisha uhusiano wa kindugu na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Burkina Faso, pamoja na kuunga mkono ajenda pana ya Umoja wa Afrika ya kuhimiza mshikamano, maendeleo na utangamano wa bara zima.
3