Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa IPU Dk. Tulia Ackson ameweka wazi kuwa mashindano ya riadha ya Betika Mbeya Tulia Marathon ni mashindano ya kipekee hapa nchini.
Dk. Tulia amesema mashindano hayo ni ya kipekee kwa sababu yanafanyika siku mbili na yanatoa fursa kwa aina zote za wakimbiaji ambapo siku ya kwanza zinafanyika mbio za ndani ya uwanja na Siku ya pili zinafanyika mbio ndefu (full marathon).
"Mbio hizi ni zakipekee kabisa kwa sababu nchi nzima hakuna mbio kama hizi, mbio ambazo tunakimbia siku mbili kwa sababu tunataka kutoa fursa ya aina zote za wakimbiaji" amesema Dk. Tulia
Ameendelea kusema kwanza tunaanza na wakimbiaji wanaokimbia hapa Uwanjani 100m, 200m, 400m, 800m na 1500m, Jana tulikuwa na Mchezo wa Kuruka kwa hiyo hizi ni Mbio za kipekee, siku ya pili huwa tunakuwa na mbio ndefu kilomita 42, 21, 10, na 15.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED