Mnyika: Hatutabaki kumlilia Lissu tunaendeleza 'no reforms no election'

By Enock Charles , Nipashe
Published at 12:27 PM May 10 2025
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu
PICHA: MTANDAO
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema pamoja na kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu yupo gerezani hawatabaki kumlilia bali wataendelea na mapambano ya kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Akizungumza na wananchi mkoani Kagera jana, Mnyika amesema wataendelea kudai haki za Lissu kupitia mahakama lakini wakati huo huo wataendeleza kampeni yao ya ‘no reforms no election’ yaani bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

CHADEMA ipo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa katika mwendelezo wa kampeni yake ya 'no reforms no election' kwa lengo la kudai mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi nchini ambayo kimedai haiko sawa.