Wenje awakataa G55, ashangaa kuhusishwa nao

By Enock Charles , Nipashe
Published at 09:20 AM May 11 2025
Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje
PICHA: MTANDAO
Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje

Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje amewataka wanachama wa CHADEMA kuendeleza kampeni ya ‘no reforms no election’ bila kujali upinzani uliopo ndani na nje ya chama hicho ili kupata mabadiliko ya kweli.

Akiongea na wananchi mkoani Geita, Wenje ambaye amekanusha kuwaunga mkono G55 amesema CHADEMA haipaswi kuendelea kuvumilia mfumo wa uchaguzi uliopo.

Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika alimtaka Wenje kuthibitisha mbele  ya wananchi wa Geita kwamba hatahama katika chama hicho licha ya kwamba alikuwa mojawapo ya watu waliomuunga mkono Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Freeman Mbowe.

“Mimi ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria hiki chama kimebeba matumaini ya watu wengi mimi mwenyewe kaka yangu amekufa kwa sababu ya CHADEMA familia yetu tuna maumivu” amesema Wenje