Waziri Mkuu ashiriki dua kuliombea taifa

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 09:26 PM May 10 2025
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
PICHA: MPIGAPICHA WETU
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amelipongeza Baraza la Waislamu Tanzania(BAKWATA) kuendelea kusimamia amani na utulivu nchini kwa kuliombea Taifa na Viongozi wake kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Hayo ameyasema leo Mei 10,2025 jijini Dar es Salaam katika kilele cha Dua Maalum ya siku tatu iliyoandaliwa na Baraza la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Ofisi ya Mufti. Waziri Majaliwa amesema dua hizi ni alama tosha ya kuona vyombo vya dini kuleta mshikamano na ushirikiano wa dhati na Serikali katika kuisimamia amani nchini.

"Dua hizi zimeunganisha waislamu wote na kuwa wamoja ikiwemo na kuwaandaa kulinda umoja na amani iliyopo kuelekea uchaguzi Mkuu na imani yangu nchi yetu tutaendelea na duru na amani na hakutakuwa na machafuko yoyote" amesema

Aidha amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia watembee kifua mbele kwakuwa taifa liko imara na hakuna shida yoyote wa uvunjifu wa amani.Mufti wa Tanzania Abubakary Zuberi Mbwana amesema wao kama wasimamiaji amani nchini ni wajibu wao kuwakusanya waumini na viongozi wa dini kutoka sehemu mbalimbali za nchi ili kuliombea taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akimuwakikisha Mkuunwa Mkoa amesema Dar es Salaam jambo la kuliombea taifa na viongozi wa dini waliotangulia ni ishara njema ya kuwa nchi iko salama na itaenda kuwa salama nyakati zote kutokana na maombi ya kina yaliyofanywa na Bakwata.

Amesema viongozi hao wa dini ambao wamekusanyika kutoka mikoa yote Tanzania kukuombea taifa inaashiri uchaguzi utakuwa na amani na utulivu.Mwenyekiti wa Kamati Dua ya kuliombea Taifa, Mwantumu Mahiza amesema dua hiyo ina maana kubwa hasa kuliombea Taifa la Tanzania kwani hakuna nchi bila amani.