Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imekabidhiwa rasmi jukumu la kutekeleza mradi wa kuunganisha umeme katika vitongoji 105 vya Mkoa wa Mbeya.
Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 10.9 na unatekelezwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambapo unatarajiwa kunufaisha takribani wateja 3,465.
Makabidhiano rasmi ya mradi huo yalifanyika katika Kata ya Igawilo, jijini Mbeya, mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dk. Tulia Akson.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED