Mamlaka ya anga ya nchini India imesitisha safari za ndege kwa muda kutokana na mashambulizi ya makombora kutoka kwa jirani yake Pakistan huku pande zote zikishutumiana.
Televisheni ya taifa ya Pakistani na idara ya uhusiano wa umma ya jeshi zimesema kuwa mashambulizi dhidi ya India yameanzishwa, baada ya kuishutumu Delhi kwa kurusha makombora katika vituo vitatu vya ndege vya Pakistan.
Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Pakistani (ISPR), Pakistan imeita mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi "Operesheni Banyan Marsus".
India haijatoa maoni yoyote kuhusu hatua hiyo.Maeneo yaliyoathirika na usitishaji huo nchini humo ni pamoja na Bathinda, Kandla, Sarasa, Uttarlai, Shimla, Ambala, Adhampur na Jamnagar
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED