MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamepokea, kujadili na kupitisha pendekezo la kugawa Jimbo la Solwa, kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Solwa na Itwangi.
Wamepitisha pendekezo hilo jana, Machi 11, 2025 kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya pendekezo la kugawa Jimbo la Solwa.
Kwamba kuwe na majimbo mawili ya uchaguzi, Solwa na Itwangi, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashaur
Amesema Jimbo la Solwa, kwa sasa linakadiriwa kuwa na watu 503,167 kufikia 2025, kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, jimbo hilo lilikuwa na watu 468,611.
“Jimbo la Solwa kwa sasa lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 4,212, likigawanywa, Solwa itabaki kuwa na kilomita za mraba 2,573.29, na Jimbo la Itwangi, litakuwa na Kilomita za Mraba 1,638.71,”amesema Oscar.
Ameendelea kueleza kuwa, Jimbo la Solwa litakuwa na Tarafa ya Nindo pamoja na Kata 12; Itwangi itakuwa na Tarafa mbili ya Itwangi na Samuye na kwamba Samuye ina Kata 4; Itwangi Kata 10 jumla zitakuwa Kata 14.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon, amesema mapendekezo hayo ya kuligawa Jimbo la Solwa ni mchakato wa awali, na kwamba mara baada ya madiwani kumaliza kuyapitisha, yatawasilishwa tena kwenye Kikao cha Kamati cha Ushauri wilaya (DCC) na kisha kwenda kwenye Kikao cha Kamati cha Ushauri Mkoa (RCC), na baada ya hapo Katibu Tawala Mkoa atawasilisha kwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.
“Vigezo vyote ambavyo vimetolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kuligawa Jimbo hili la Solwa tumekidhi, tuombe Mungu ligawanywe na nitafurahi kuona Madiwani mkijitokeza kugombea Ubunge katika Jimbo hili jipya la Itwangi sababu nyie ndiyo mnajua zaidi changamoto za wananchi,” amesema Simon.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Edward Ngelela, ameipongeza INEC, kwa nia ya kuligawa Jimbo la Solwa na kwamba itasaidia kusogeza huduma kwa wananchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED