Makalla: Samia ni karata muhimu CCM uchaguzi tunaouwendea

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 11:29 AM Jun 11 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, amesema CCM kinakubali kazi za Rais Samia Suluhu Hassan na kinamwona ni karata muhimu katika uchaguzi wanaouwendea.

Ametoa kauli hiyo leo Juni 10,  2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi Vijijini,mkoani Kilimanjaro

Amesema CCM kinakubali kazi za Rais Samia  na kinamwona ni karata muhimu katika uchaguzi wanaouendea.

“Chama Cha Mapinduzi halitapata shida ya kufanya kampeni kubwa kueleza mambo yaliyofanywa kwa sababu tunajivunia kazi alizofanya zinaonekana katika vitongoji na vijiji, mitaa na kata,” amesema.

Makalla amesema Rais Samia kiila mahali ameweka alama za maendeleo ujenzi wa madarasa, miradi ya maji, barabara, umeme na utalii ameukuza mikoa ya Kaskazini ambapo kabla ya filamu ya The Royal Tour watalii walikuwa 46,000 lakini hadi Aprili, mwaka huu walifikia 92,000 na sasa ni zaidi ya 100,000.

“Rais Samia ameingia katika historia kupeleka fedha nyingi na Chama Cha Mapinduzi kinamwona ni karata muhimu ya ushindi wa CCM, hivyo, CCM hatutapata shida ya kufanya kampeni kubwa kueleza mambo yaliyofanywa kwa kuwa, tunajivunia kazi alizofanya zinaonekana katika vitongoji, vijiji, mitaa na kata,” amesema.