Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026 kusomwa leo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:36 PM Jun 12 2025
Bajeti Kuu ya Serikali 
2025/2026 kusomwa
 leo
Picha:Nipashe Digital
Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026 kusomwa leo

Bajeti hiyo inatarajiwa kuanza kusomwa kuanzia saa 10:00 jioni bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

Ikumbukwe, mapema mwezi Machi mwaka huu, Dk.Nchemba aliwasilisha mapendekezo ya mfumo na ukomo wa bajeti hiyo bungeni Dodoma mbele ya Kamati ya Bunge zima iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Serikali ilipendekeza ukomo wa bajeti wa shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo ukomo huo ni sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya shilingi trilioni 50.29 ya mwaka 2024/2025 unaomalizika Juni 30 mwaka huu.

Dk. Nchemba alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni pamoja na kuendelea kuzingatia maeneo makuu ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa miaka mitano ambao ni kuchochea uchumi shindani na shirikishi, kuimarisha uzalishaji wa bidhaa viwandani, utoaji huduma, kukuza uwekezaji, biashara, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu.