Makamu wa Rais Zanzibar anyimwa kiwanja kufanya mkutano Shinyanga

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:18 PM May 22 2025


Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
Picha: Mtandao
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amenyimwa kutumia Kiwanja cha Nguzo Nane kinachomilikiwa na Jeshi la Zimamoto kufanya Mkutano wake wa hadhara Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Othman Masoud ana ziara kwenye majimbo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa akianzia na Jimbo la Shinyanga Mjini tarehe 24 Mei 24, 2025.

Kwenye taarifa yake Jeshi la Zimamoto inasema kuwa Mkutano wa Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud umepigwa marufuku kufanyika viwanja hivyo kwa sababu viwanja vya Jeshi havitumiki kwa shughuli za kisiasa.

Hata hivyo, kwa upande wake, Naibu Katibu wa Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo anasema kuwa taarifa hiyo ya Jeshi la Zimamoto haina msingi wowote kwa sababu marufuku ya viwanja vya Jeshi inahusu viwanja vya ndani ya kambi za Jeshi na sio viwanja vya wazi vinavyomilikiwa na Jeshi. Amesema viwanja hivyo vimetumika mara nyingi kwa shughuli za kisiasa na zuio la sasa linakusudia ķuhujumu ziara ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar.