Mambo matatu likiwemo la hamahama ya makada wa chama hicho yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA inayotarajiwa kuketi kuanzia kesho jijini Dar es Salaam.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa kikao hicho cha hadhi ya juu katika chama kukaa bila uwepo wa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, suala la hamahama ya makada wa chama hicho linatarajiwa kuwa mojawapo ya jambo la mjadala katika kikao hicho ili kulipatia ufumbuzi.
Suala la kesi mbalimbali zinazokiandama chama hicho ikiwamo kesi inayomkabili Mwenyekiti wake wa chama taifa na pia kesi dhidi ya chama hicho iliyofunguliwa na baadhi ya viongozi wastaafu wa chama hicho upande wa Zanzibar linatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho.
Licha ya masuala hayo pia lipo suala la kampeni ya chama hicho maarufu ya ‘No reforms no election’ ambayo imekwisha kufanyika katika mikoa mbalimbali hapa nchini na ambayo inatarajiwa kuendelea linaweza kuwa suala la mjadala katika kikao hicho.
Licha ya mafanikio yake lakini kampeni hiyo inahitaji fedha za kutosha ili kuiendeleza jambo ambalo wadau mbalimbali pamoja na wanachama watahitajika kuendelea kuichangia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED