Mchungaji kuchapisha ushuhuda ni kosa kisheria

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 03:17 PM Mar 23 2025
news
Vitus Audax
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taarifa Binafsi (PDPC) Dk.Emmanuel Mkilia akifungua semina ya waandishi wa habari juu ya matumizi ya taarifa binafsi.

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), imesema utaratibu wa wachungaji na watumishi kuweka hadharani taarifa binafsi za waumini wao katika vyombo vya habai na mitandao ya kijamii kwa kigezo cha ushuhuda ni kinyume cha sheria n ani hatari kwa mtakhabari wa Maisha binafsi ya mhusika.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 23,2025 na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Innocent Mungy wakati akitoa semina kuhusu siri za mtu na taarifa binafsi na umuhimu wa kuzihifadhi kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza.

Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Innocent Mungy
Vilevile, Mungy amesema kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi namba 11 ya mwaka 2022 endapo mchungaji akichapisha taarifa binafsi za muumini bila idhini yake anayo haki ya kumshtaki na kulipwa fidia.

“Muumini anayo haki ya kumshitaki mchungaji endapo taarifa za ushuhuda wake zimewekwa hadharani bila idhini yake na sisi kama tume tutashughulikia taratibu zote hadi anapata fidia hiyo kwani ni kinyume cha sheria kuweka taarifa binafsi za mtu,” anasema.


Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dk.Emmanuel Mkilia amesema tume hiyo imeongeza muda hadi kufikia Aprili 30, 2025 taasisi zote kuhakikisha zinajisajili na kuwasilisha maombi ya matumizi ya taarifa binafsi ili kulinda utu wa wananchi.