"Midoli matangazo nguo za ndani inadhalilisha wanawake"

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 08:13 PM Jun 16 2025
CCM yasema midoli kuuzia nguo inadhalilisha wanawake, washauri serikali kuingilia kati.

Baraza la Wazazi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limeishauri serikali kutoa mwongozo wa namna bora ya matangazo ya biashara za nguo za ndani za wanawake kwa kutumia midoli, ambayo imetajwa kuchochea mmonyoko wa maadili katika jamii.