Mirembe yaja na mwongozo wa tiba ya saikolojia

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 05:42 PM Mar 06 2025
Mkurugenzi wa hospital ya taifa ya afya ya akili Dk. Paul  Lawala.
Picha:Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi wa hospital ya taifa ya afya ya akili Dk. Paul Lawala.

Mwongozo wa elimu ya saikolojia kwa wagonjwa wa skizofrenia na ndugu zao utatambuliwa rasmi kwenye miongozo ya tiba ili kuelimisha jamii kuhusiana na afya ya akili.


 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa hospital ya taifa ya afya ya akili Dk. Paul  Lawala wakati wa Kikao kazi cha na wadau wa Utafiti uitwao KUPAA  kwaajili ya uboreshwaji wa huduma na elimu ya afya ya akili kwa wagonjwa na zao.
 
Amesema uwepo wa mwongozo wa huduma za wagonjwa wa skizofrenia utasaidia kutambua wagonjwa pamoja na familia zao na kusaidia watu wanaoumwa au watakaoumwa baadaye.
 
“Utafiti huu utasaidia namna gani huduma hizi za wagonjwa wa skizofrenia pamoja na familia zao zinaweza zikapata kutambuliwa rasmi kwenye miongozo ya tiba na kusadia watu ambao wanaumwa na wengine ambao pengine watakuja kuumwa,”amesema Dkt. Lawala
 
Aidha, amesema kwenye nchi zilizoendelea kuna miongozo ambayo inaota kama afua, muongozo wa saikolojia kwa familia na wagonjwa sasa kwa wanaojua kuwa miongozo inasaidia kusema nini kifanyike na kwa utaratibu gani kwa kundi fulani la wagonjwa.