WAKATI jina la Prof. Mohamed Janabi, likitangazwa rasmi kuwa miongoni mwa wagombea watano katika kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ajaye wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Kanda ya Afrika.
Nipashedigital, imekuandalia wasifu kitaaluma wa mtaalamu huyo wa afya, kwa miongo kadhaa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, limetoa taarifa hiyo, jana. Majina ya wagombea hao ambayo yatafanyiwa mchakato wa Uchaguzi Mei 18, mwaka huu, yaliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.
PROF. JANABI NI NANI?
Prof. Janabi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhinbili (MNH), tangu mwaka 2022 hadi sasa.
Ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye masuala ya afya nafasi aliyoteuliwa miezi michache iliyopita.
Mwanataaluma mbobezi katika sekta ya sayansi ya tiba akiwa na shahada tatu: Shahada ya Awali ya Udaktari wa Tiba (MD); Shahada ya Uzamili ya daktari (MSc); Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Tiba (PhD).
Pia amebobea kwenye utafiti na tiba, pia zinazotumika duniani kote. Kadhalika, Prof. Janabi ni mhadhiri Mshiriki ma Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo cha Marekani (EACC) na Mkaguzi wa Matibabu wa Usafiri wa Anga aliyeidhinisbwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA-USA).
Kabla ya kwa Mkurugenzi Mtendaji MNH, Prof. Janabi amefanya kazi ya kibobezi katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2022.
Kuanzia mwaka 2005 hadi sasa amekuwa Daktari Mkuu wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, pia Prof. Janabi ni Mhadhiri Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia mwaka 2000 hadi sasa.
Pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tiba cha South Carolina, Marekani kuanzia mwaka 2003 hadi sasa.
Prof. Janabi anahudumu kama mjumbe wa Bodi kwenye taasisi kubwa za huduma ya tiba nchini zikiwamo, JKCI, Taasisi ya Sratani ya Ocean Road (ORCI), MUHAS, Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA).
Kadhalika, amekuwa Mwanasayami Mwandamizi wa Majaribio ya Chanjo ya Ukimwi (TaMoVac) kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2002 na Daktari Mkurugenzi katika Shirika lisilo la Kiserikali la Madaktari wa Afrika lenye asili yake Marekani.
Kwa miaka mingi ya utumishi wake kwenye tasnia ya sayansi ya tiba ndani na nje ya Tanzania, amejihusisha ma tafiti nyingi na amefanikiwa kutoa machapisho 83.
Chapisho la ‘Mtindo wa Maisha na Afya Yako’, ni juhudi zake binafsi, kuhamasisha Watanzana kutambua jambo moja kubwa kuhusu afya zao.
Anazungumza na kuandika vyema lugha nne za kimataifa ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kirusi na Kijapan.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED