Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 09:07 PM Mar 15 2025
Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai
Picha: Mpigapicha Wetu
Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai

Wanawake wawili wanaodhaniwa kuwa washirikina wamekamatwa alfajiri hii wakiwa watupu katika madhabahu ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Tukio hili limeleta taharuki kubwa baada ya wanawake hao kudai walitumwa kuchukua ulimi wa marehemu aliyezikwa hivi karibuni katika makaburi ya usharika.

Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na wanawake hao wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

Mwinjilisti wa Usharika wa Nkwarungo, Jeremiah Nkya, alisema walinzi walikamata wanawake hao wakiwa na mabunda ya vitu visivyoeleweka.