MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshusha tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere Kigamboni, Dar es Salaam, kwa usafiri wa pikipiki na bajaji kutoka Sh. 1,500 na sasa Sh. 500 kwa bajaji Sh.300 pikipiki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema awali pikipiki na bajaji zilikuwa zikitozwa Sh. 1,500.
Amesema lengo la serikali ni kuwaondolea kero wananchi wa Kigamboni ambao walikuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu viwango vya tozo walizokuwa wakilipa wanapovuka darajani.
Amesema wastani wa makusanyo ya mapato kwa mwezi kwenye daraja hilo yameongezeka kutoka Sh. bilioni 1.13 kwa kipindi cha Februari 2021 hadi kufikia wastani wa Sh. bilioni 1.89 katika kipindi cha Februari 2025, sawa na ongezeko la asilimia 66.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED