Waliojiajiri kuweka michango NSSF kuzinduliwa skimu yao

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:15 PM Mar 17 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema mfuko huo unatarajia Aprili mwaka huu, kuzindua skimu ya uchangiaji wa hiari kwa wananchi waliojiajiri ambayo imefanyiwa maboresho.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo, jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mshomba amesema katika mpango huo, wananchi waliojiajiri kwenye sekta mbalimbali watapata huduma za hifadhi ya jamii kama wanavyonufaika wanachama walioajiriwa katika sekta rasmi.

“Hadi kufikia Februari 2025, wanachama 437,319 wamejiunga kwenye skimu hii na wanaendelea kunufaika na mafao kama pensheni ya uzeeni, urithi, uzazi, matibabu, ulemavu na fao la kujitoa. 

“Skimu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Aprili 2025,” amesema.