CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya majadiliano.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia, ajenda kuu ya kuitwa kwa chama hicho ni kujadili kauli mbiu ya ‘No reform no election’.
“Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), kinapenda kuwataarifu viongozi, wanachama na Watanzania kwa ujumla kuwa, kesho, Jumanne saa nne asubuhi.
“Kitakutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuitikia wito wake, ajenda kuu ya wito huo ikiwa ‘No reform, no election’.
“Katibu Mkuu, John Mnyika ataongoza ujumbe wa chama kwenda kuonana na Msajili wa Vyama vya Siasa, kisha chama kitatoa mrejesho rasmi kwa wanachama na umma kwa ujumla baada ya kikao hicho,” imeeleza taarifa hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED