MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema tayari mfuko huo umepeleka mapendekezo kwa serikali ya marekebisho ya sheria, ili kuruhusu mtu anapotoka kazini alipwe mafao yao ndani ya miezi mitatu na si kusubiri kwa miezi 18.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mshomba amesema;
“Tumefanya tathmini kwa kutumia wataalamu wetu wa ndani, ili kuona mfuko utaathirika vipi na maamuzi ya kuwalipa wanaotoka kazini, ikaonekana tunaweza kufanya hivyo, sasa tumewasilisha mapendekezo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, ili wanaotoka wanalipwa mafao yao bila kusubiri miezi 18.”
Amesema tathmini inaonesha mfuko hautaathiriwa kwenye ulipaji mafao kwa wastaafu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED