Program utunzaji nishati kuleta mapinduzi ya kiuchumi Tanzania

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 05:16 PM Mar 17 2025
Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda (watatu kulia) na Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Kimataifa na Diaspora wa Ireland, Neale Richmond (wanne kulia)wakikagua maabara yenye vifaa vya kisasa vinavyotumika kufunzishia wanafunzi wa prrogramu ya utunzaji nishati
Picha: Mauld Mbagga
Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda (watatu kulia) na Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Kimataifa na Diaspora wa Ireland, Neale Richmond (wanne kulia)wakikagua maabara yenye vifaa vya kisasa vinavyotumika kufunzishia wanafunzi wa prrogramu ya utunzaji nishati

MWAKILISHI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Shigeki Komatsubara, amesema program ya utunzaji wa nishati itasaidia kuleta mapinduzi kwa taifa linalokuwa kiuchumi kama Tanzania, na kwamba uwekezaji uliofanyika utaenda kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo wakati Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Kimataifa na Diaspora wa Ireland, Neale Richmond, alipotembelea Chuo cha Teknolojia (DIT) kwa lengo la kujionea maendeleao ya wanufaika wa program ya mafunzo maalumu ya utunzaji wa nishati, unaofadhiliwa na UNDP, Umoja wa Ulaya (EU) na Ireland.

Amesema prograni hiyo itakuwa mkombozi wa kuleta mabadiliko kwa kuifanya Tanzania kukuwa kiuchumi, kwakuwa nishati itakayo okolewa itaenda kutumika katika kuendesha masuala mengine ya kimaendeleo.

“Naishukuru serikali ya Tanzania, EU, na Ireland kwa kushirikiana na UNDP katika kutekeleza mpango huu ambao pia utaenda kuimarisha hali ya kimaisha ya watanzania, pamoja na kuwainua wanawake katika sekta ya teknolojia,” amesema Komatsubara.

Mmoja wa wanufaika wa program hiyo Salma Liogope, amesema kutokana na ujuzi wa namna ya kufanya ukaguzi na matumizi bora ya nishati, utaenda kuwasaidia kupunguza matumizi ya umeme katika sekta mbalimbali, hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa umeme uliokuwa ukipotea bila sababu.

“Taifa halina shida katika uzalishaji wa umeme lakini tatizo linakuja ni jinsi gani unatumika, kusipokuwa na elimu ya matumizi sahihi uzalishaji huo hautakuwa na maana, kwahiyo tunashukuru kupatiwa mafunzo hayo kwasababu tutaenda kuielimisha jamii kujua ni kifaa gani sahihi akitumie ili kupunguza matumizi, na kuokoa gharama,” amesema Gladys.

Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda (watatu kulia) na Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Kimataifa na Diaspora wa Ireland, Neale Richmond (wanne kulia) wakikagua maabara yenye vifaa vya kisasa vinavyotumika kufunzishia wanafunzi wa prrogramu ya utunzaji nishati katika Chuo cha Teknolojia (DIT) ambayo inayofadhiliwa na UNDP, EU na Ireland. Wakwanza kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UNDP Shigeki Komatsubara. Picha Maulid Mmbaga.