MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Joyce Shebe amesema wanawake watakaoonesha nia ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 wanapaswa kuungwa mkono na jamii ili waweze kutimiza ndoto zao za kuwa viongozi.
Ushauri huo ameutoa leo Jijini Dodoma katika Mkutano wa wanachama waTaasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA - TAN) na wadau wa habari,ambapo amesema Mwanamke hapaswi kukatishwa tamaa pindi anapotaka kuomba nafasi mbalimbali katika uchanguzi mkuu.
Mwanamke asihukumiwe kwa jinsia yake na badala yake ahukumiwe kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake katika nafasi aliyonayo na uchaguzi usitumike kama kigezo cha kumkandamiza ili asipate haki ya kikatiba ya kuchaguliwa.
"Wanawake wamekuwa waoga kujitokeza kugombea katika chaguzi mbalimbali kwa hofu ya kudhalilishwa,wakiwa majukwaani hivyo ni budi jamii iondokane na dhana hizi kandamizi ambazo sisi TAMWA tumekuwa tukizipinga,"amesema Shebe.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED