Msomi ashauri jamii kutunza historia kwenye vitabu

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 07:53 PM Mar 23 2025
Msomi ashauri jamii kutunza historia kwenye vitabu
Picha: Mpigapicha Wetu
Msomi ashauri jamii kutunza historia kwenye vitabu

PROFESA wa Historia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Frederick Kaijage, amesema ni vyema jamii ikajenga utaratibu wa kuandika vitabu kuwahusu wao maishani, ili kujenga historia na kuacha kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Prof. Kaijage, mwanataaluma aliyebobea katika historia, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa u kitabu kiitwacho; ‘Maisha ya Omwami Evarista Kashaga’, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

“Duniani kwa watu kuna kitu tunaita utambulisho, ndio kitu muhimu. Kwa sababu wewe ukiwa hapa (duniani), unafikiri wewe ni nani? Umetoka wapi? Watu wanoishi na ambao wamekwishaondoka una uhusiano gani nao?

“Jaribu kujielewa wewe mwenyewe chimbuko lako, kitu kinachokutambuliosha ni kitu kipi. Mimi naweza kujitambulisha ni Profesa, maana yake nini? Sawa kwa wanataaluma wenzangu.

“Wataona ni muhimu sana. Lakini mimi ni mtoto wa Kaijage, huo ni utambulisho zaidi kuliko vitu vilivyokuja baadae, historia yao, jitambue, jielewe, jitambulishe,” amesema Prof. Kaijage.

Amesema hatua ya kujitambua ndio msingi wa watu kutambuana, na kwamba koo mbalimbali zilizomo duniani si kitu cha kupewa bali huendana na vinasaba vya jamii ya kundi fulani.

“Vinasaba vyako ndio wewe, ndio ukoo wako. Kuna sehemu ukitembea utakutana na koo fulani. Kuandika kuhusu koo fulani si kwamba ni ukabila, ni kwa lengo la kutambuana, mshikamano na upendo. Utaifa utatambulishwa na wahusika, ila kuhusu ukoo ni wewe mwenyewe,” ameongeza mwanataaluma huyo..

Awali, Mwandishi wa Kitabu hicho, ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) nchini, Dk. Frateline Kashaga, amesema kwamba lengo la uandishi wa kitabu hicho ni kutunza kumbukumbu kwa kuwa walio wengi hutunza historia zao kwa hadithi.,

Amesema ingawa Watanzania wenye nia ya kutunza historia vitabuni, hata kwa mfumo wa kisasa kidijitali bado hukumbwa na changamoto kadhaa ikiwamo uchumi duni.

“Pamoja na changamoto zilizopo kutunza kumbukumbu za familia ni utamuduni mzuri. Kuhusisha watafiti, wataalamu wa lugha, wadau wa ili kufadhili, itafanikisha hilo, kusaidia jamii zetu kuacha urathi,” amesema Dk. Kashaga.