Muhimbili kushughulika na vibogoyo

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 04:32 PM Mar 06 2025
Meno
Picha: Mtandao
Meno

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imeanzisha matibabu ya kuziba mapengo, huku mzizi bandia hupandikizwa kwenye taya, kisha kuwekewa meno juu yakigandishwa na kutumika kama sehemu ya meno ya kuzaliwa nayo.

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH, Dk. Rachel Mhavile, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dk. Mhavile, amesema huduma hiyo ya kupandikiza meno kwenye taya, kwa kutumia mizizi bandia, inapunguza usumbufu kwa watu wenye shida ya mapengo, ambao wanatumia meno bandia ya kuweka na kutoa.