Afungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka sita

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:41 PM Jun 26 2025
Nyundo ya Mahakama.
Picha: Mtandao
Nyundo ya Mahakama.

Mrisho Mussa Nchemba (31) Mkulima mkazi wa Milama, Kata ya Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro , amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka 6.

Akisomewa hukumu hiyo Juni, 25, 2025 mbele ya Mheshimiwa Hakimu George Ngowi wa Mahakama ya Wilaya ya Mvomero ambaye alieleza, Mnamo Novemba 28, 2024 majira ya saa 2 asubuhi Mshitakiwa Nchemba alimvizia muhanga akiwa amelala kisha kuingia ndani ya nyumba, kumbaka na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema, vitendo hivi vya Ukatili vinasababishwa na mmomonyoko wa maadili kwenye jamii husika, hivyo mbali na kuchukua hatua za kisheria, Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madhara ya vitendo vya ukatili.

Chanzo: Dawati la habari polisi Morogoro