Wenye mahitaji maalum wapewa vifaa saidizi kuadhimisha kuanzisha WCF

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 08:07 PM Jun 26 2025
Wenye mahitaji maalum wapewa vifaa saidizi kuadhimisha kuanzisha WCF
Picha: Mpigapicha Wetu
Wenye mahitaji maalum wapewa vifaa saidizi kuadhimisha kuanzisha WCF

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amekabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba Singida.

Akikabidhi vifaa hivyo jana ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni pamoja na viti mwendo 46,fimbo nyeupe 154 na limu paper maalumu 200 ambavyo vilikabidhiwa kwa uongozi wa chuo hicho, alisema Serikali itahakikisha inaweka mazingira bora kwa watu wenye ulemavu kupata elimu bila vikwazo ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk. John Mduma, alisema mfuko huo unaadhimisha miaka 10 kwa kuwasaidia watu wenye ulemavu kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake na kwamba WCF itaendelea kuwekeza katika jamii kupitia sera yao ya kurudisha kwa jamii ili kuhakikisha Watanzania wote bila kujali hali zao wananufaika na uwepo wa taasisi hiyo.