Mahakama ya Hakimu Mkazi imemhukumu kifungo cha maika 30 jela mshtakiwa Saidi Idd Rajabu (21) fundi msaidizi mkazi wa Mkazi wa Tambuka reli Manispaa ya Morogoro kwa kosa la Kumbaka mwanafunzi wa miaka 14.
Hukumu hiyo imetolewa Juni 25, 2025 chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ester Ushaki wa mahakama hiyo iliyopo Kihonda Morogoro Manispaa.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Ushaki amesema, Mshtakiwa huyo ambaye ni fundi msaidizi wa kazi za ujenzi alifanya tukio hilo Februari 12, 2024 majira ya saa 12 jioni, huku akitumia mbinu ya kumlaghai kwa maneno mtoto huyo na kwenda naye nyumbani kwake kisha kumbaka.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema, mshtakiwa alitafutwa na kukamatwa siku chache baada ya taarifa hiyo kufika kituoni na kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha, Kamanda Mkama ametoa wito kwa vijana kuacha tamaa za mwili zinazopelekea kufanya vitendo vya uikatili wa wanafunzi na watoto.
Dawati la habari polisi Morogoro
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED