Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Mhandisi Stephen Wangwe amesema endapo taarifa binafsi za mtu zikiwemo picha zikitumika katika kufanya tangazo la kitu chochote bila idhini yake anayo haki ya kushitaki na kulipwa fidia chini ya usimamizi wa wa Tume hiyo.
Wangwe amebainisha hayo wakati wa semina ya jinsi ya kuripoti habari zinazohusu taarifa binafsi kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza na kueleza kuwa tume hiyo itagharamika kuhakikisha kila mtanzania taarifa zake zinalindwa.
Amesema picha, majini, umri pamoja na taarifa nyingine binafsi hazitakiwi kutolewa bila idhini ya mhusika na kwa matumizi yanayotambulika kwa mujibu sheria na kuwa endapo muhusika taarifa zake zikitumika bila idhini yake anaweza kushita katika tume hiyo.
Amesema mhusika anaweza kutoa malalamiko yake kwa kufuata taratibu ambazo ni pamoja na kuwasilisha malalamiko katika mfumo rasimi wa tumie hiyo unaopatikana mtandaoni.
“Hatua ya pili mchakato utafanyika kwa siku saba ili kubaini mashiko ya malalamiko hayo, Tume itamuita mtumia taarifa ili alete utetezi wake ndani ya siku 20 baada yah apo tume itanza uchunguzi,”
“Baada ya uchunguzi tume itawaita wote wawili kusikilizwa, itatwa kamati kwaajili ya kupitia malalamiko husika na kutolewa maamuzi. Atakayeona ameonewa anasiku 14 za kukata rufani,” amesema
Aidha, amesema baada ya hatua hiyo ya kukata rufani, kamati itabadilishwa na wateuliwa watoa hukumu wapya na endapo mhusika hatoridhika shauri litapelekwa mahakamani chini ya usimamizi wa Tume hiyo ili kuhakikisha haki inapatikana.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED