WACHIMBAJI wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, wameianguka serikali kuwasaidia kuapata nishati ya umeme migodini.
Wamesema hatua hiyo ni kupunguza gharama za uendeshaji, kukuza uchumi wao na kuongeza maduhuri ya serikali wakati wa masoko.
Ombi hilo, limeliwasilisha wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, kutembelea migodi midogo, kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo, wakisema gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa kwa sababu wanatumia mfumo wa majenereta.
Amesema mgodi wa Nyamishiga unaosimamia ukusanyaji wa maduhuri ya serikali yamekuwa yakishuka kila siku na sasa wanakusanya Sh. milioni tatu hadi nane kwa mwezi kutoka Sh. milioni 70 kwa sababu ya wachimbaji wengi wamehama na kuelekea kwenye migodi yenye maji.
Katibu wa Mgodi wa Kasi Mpya, Hosea Mbusule amesema, transfoma ya umeme iliyopo haikidhi mahitaji ya mgodini kulingana na wingi wa mashine zilizopo na kuna wakati inawakata moto na kusababisha kusimama kwa uzalishaji au kutumia njia mbadala ya genereta.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhita, amesema migodi yote midogo isiyokuwa na nishati ya umeme atahakikisha inapata huduma hiyo ili kuwaondolea gharama za uzalishaji, na kuwataka viongozi kuendela kudhibiti utoroshaji wa madini, ili serikali isikose mapato yake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED