Wanafunzi, Wauguzi Kolandoto wameadhimisha siku ya wauguzi duniani

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 12:54 PM May 16 2025
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Paschal Shiluka akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani katika Chuo hicho.
PICHA: MARCO MADUHU
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Paschal Shiluka akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani katika Chuo hicho.

WANAFUNZI wa kada ya Uuguzi kutoka Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kilichopo mkoani Shinyanga, wameadhimisha siku ya wauguzi duniani kwa kufanya pia matendo ya huruma kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Kolandoto, kama sehemu ya kumuenzi Muuguzi wa kwanza duniani Florence Nightingale.

Maadhimisho hayo yamefanyika jana Mei 15, 2025. Mkuu wa Chuo hicho Paschal Shiluka,amewapongeza wanafunzi wa Kada hiyo ya Uuguzi chuoni hapo, kwa kuadhimisha siku ya uuguzi duniani, ambapo mara nyingi wamekuwa wakiona wanaoadhimisha ni wale waauguzi ambao tayari wapo kazini.

Amewataka wanafunzi hao,kwamba watakapohitimu masomo yao na kuwa kazini,waipende taaluma yao,wazingatie maadili pamoja na kufanya kazi kwa weledi katika kuhudumia wagonjwa, ili wamuenzi kwa vitendo Muuguzi wa kwanza Duniani Frolence Night Ngale.

“Nawapongeza Wanafunzi Wauguzi katika Chuo hicho cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kuadhimisha siku ya Wauguzi Duniani na kumuenzi Muunguzi wa kwanza Duniani Frolence Night Ngale hii inaonyesha kwamba mnapenda taaluma yenu,”amesema Shiluka.

1

Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Ukunga Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Wande Kayeji,amewasisitiza wanafunzi hao kwamba watakapokuwa kazi,wawahudumie wagonjwa kwa upendo na moyo mmoja na wasijekutanguliza masuala ya rushwa.

 Naye Mwanafunzi Mwanne Hamisi Bulabo, akizungumza kwa niaba ya wenzake,amesema siku hiyo ya Uuguzi Duniani ni muhimu kwao kama wanataaluma,ndiyo maana wameadhimisha siku hiyo, ili kumuenzi Muunguzi wa kwanza Duniani Frolence Night Ngale, kwa kufanya pia na matendo ya huruma na kutoa zawadi ya vitu mbalimbali kwa wagonjwa.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto Bonaventure Matogo,amewapongeza wanafunzi hao wauguzi,kwa kuaadhimisha siku ya wauguzi duniani,na hata kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.