Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Simbachawene, ashuhudia mwanachama wa PSSSF, Susane Kimambo, jinsi anavyoweza kujihudumia kupitia simu janja, baada ya kuunganishwa na PSSSF Kidijitali.
Waziri ameshuhudia hayo wakati alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 17, 2025.
Maonesho hayo yaliyoanza Juni 16 na kuzinduliwa rasmi na Waziri Simbachawene Juni 17, yamebeba kauli mbiu isemayo “ Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji.
Akitoa maelezo kwa Waziri kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko kwa wanachama na wananchi wanaotembela banda hilo, Meneja Rasilimali Watu PSSSF, Gloria Mboya amesema, pamoja na kuwahudumia wanachama pia Mfuko unawaelimisha na kuwaunganisha wanachama na mfumo wa PSSSF Kidijitali unaowawezesha kujihudumia wao wenyewe kupitia simu janja.
Aidha Meneja huyo wa PSSSF, ameipongeza serikali na menejimemnti ya PSSSF kwa kuwajali watumishi wa Mfuko huo kwa kuhakikisha haki zao zinapatikana kwa wakati.
Maonesho hayo yanalenga kuhamasisha na kuwapa motisha watumishi wa umma waendelee na kazi yao nzuri ya ujenzi wa Taifa na kuendelea kuwa wabunifu ili kutatua changamoto mbalimbali katika jamii;
Lakini pia kupata mrejesho kutoka kwa wateja/wananchi na wadau wanaowahudumia na kuandaa Utumishi wa Umma ili uweze kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo siku za usoni.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED