HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, imeanzisha huduma za matibabu ya kufuta ‘tatoo’, kwa watu ambao wanahitaji kuziondoa katika miili yao.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk. Rachel Mhavile, amesema hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema, wameanzisha matibabu ya magonjwa ya ngozi kwa njia ya tiba mwanga (phototherapy) na tiba ‘laser’ ikiwa ni hospitali pekee nchini inayotoa huduma hiyo.
Amsema, huduma hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya vitiligo na saratani za ngozi ambapo wastani wa wagonjwa 10 hadi 15 wanahudumiwa kwa wiki wakiwamo wenye mahitaji ya kufuta tatooo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED