LICHA ya Marekani kueleza wazi kusitisha ufadhili na misaada mbalimbali ya utolewaji wa dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa Ukimwi (ARVs), kwa nchi za kiafrika ikiwamo Tanzania, imebainika kuwa kata ya Rusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera ina watumiaji 600 wa dawa hizo.
Mbali na watumiaji hao, watu wengine 35 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo pamoja na wanane ambao wamethibitika kuambukizwa magonjwa ya zinaa, kwa kipindi cha miezi mitatu pekee.
ya Diwani wa kata ya Rusahunga, Apornal Mugarula, iliyosomwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo na Diwani wa Viti Maalumu, Ziyun Hussein, huku akionesha sababu za kupaa kwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Amesema sababu kubwa ni ongezeko la vijana walioingia kwenye kata hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara, ikiwAmo ujenzi wa lami ya Rusahunga kwenda Rusumo wilayani Ngara pamoja na maegesho makubwa ya magari yanayotoka ndani na nje ya nchi.
Ametaja sababu nyingine za maambukizi ni watu kutozingatia taratibu na kanuni za kufanya ngono salama, umaskini wa vipato pamoja na tamaa ya kutoridhika na mpenzi mmoja mwaminifu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED