Wasira afanya mazungumzi na Spika wa Cuba

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 05:43 PM Mar 06 2025
Wasira afanya mazungumzi na Spika wa Cuba
Picha: Mpigapicha Wetu
Wasira afanya mazungumzi na Spika wa Cuba

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez na ujumbe wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM Wasira amefanya mazungumzo na ujumbe huo uliofika kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba,  Dar es Salaam leo Machi 6, 2025.

Katika mazungumzo na ujumbe huo kutoka Cuba wameahidi kuendeleza ushirikiano wa kihistoria kati CCM na Chama cha Kikomunisti cha Cuba, pamoja na Tanzania na Cuba.