IJUE LESOTHO ALIYOING’ONG’A TRUMP

By Beatrice Moses , Nipashe
Published at 03:18 PM May 01 2025
Mkazi wa Lesotho akiwa katika vazi lake la asili, amebebwa na farasi, nyenzo yao ya asili ya usafiri
Picha: Mtandao
Mkazi wa Lesotho akiwa katika vazi lake la asili, amebebwa na farasi, nyenzo yao ya asili ya usafiri

AKIWA na siku chache madarakani, Rais Donald Trump wa Marekani amkuja na matamshi, pia uamuzi unaotikisa dunia.

Mojawapo ni pale akiwa na siku chache madarakani, akalishambulia taifa la Lesotho, ambalo limekuwa likipokea msaada mkubwa wa Marekani, hasa kuikimu na janga kubwa la Ukimwi linaloikabili.

Hapo Rais Trump akanena akiwa Bungeni Marekani kuwa” (Lesotho) ingefaidika na dola milioni nane (Sh. bilioni 21.52) kukuza ushoga.”

Ni hatua iliyoonekana kuigadhabisha serikali ya Lesotho ikalalalamika kulikoni hayo, utu wake kudhalilishwa.

Kwa ujumla, Lesotho ni miongoni mwa wanufaika wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada katika kupambana dhidi ya Ukimwi, ambayo imekuwa ikitekelezwa na marais watangulizi.

Lesotho, pia imo katika nchi zenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya VVU duniani. Hivyo, serikali ya Marekani imekuwa ikitenga kiasi cha takriban dola bilioni moja kila mwaka tangu mwaka 2006, sawa na Sh. Trilioni 2.69 kuisaidia kukabiliana na janga hilo, ikiwamo kwa huduma za kinga, matunzo na matibabu.

Hapo pia, nchi hiyo ya Kiafrika, haipo mbali na uzalishaji mkubwa wa vitambaa vya nguo za suruali aina za ‘jeans’ vinavyovaliwa sana Marekani.

SIFA ZAKE ILIVYO  

Zifahamu sifa zake Lesotho kijamii na kimazingira kama ifuatavyo:

Ufalme wa Milimani: taifa hilo la  kifalme limeundwa zaidi na nyanda za juu na kufikia vijiji vingi nchini humo inakulazimu kutumia farasi, kutembea au matumizi ya ndege.

Hiyo inajulikana kama '' Kingdom in the Sky'', yaani nchi huru pekee duniani ambayo maeneo yake yote yako juu kwa wastani wa jumla mita 1,000 juu ya usawa wa bahari (Futi 3,281). 

Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (Futi 4,593) na zaidi ya asilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (Futi 5,906).

Lesotho inafahamika kuwa na mojawapo ya viwanja vya ndege vikubwa zaidi duniani, Uwanja wa Ndege wa Matekane, wenye njia fupi ya kuruka na kutua ndege.

Inaelezwa, hata ndege inavyopaa na kutua uwanja wa ndege huo, ni kwa kutumia ujuzi wa nafasi ndogo, kutokana na mpangilio wa ardhi ulivyo na vilima.

Kwa mipaka, imezungukwa na taifa la Afrika Kusini pande zote: Nchi hiyo inazungukwa na Afrika Kusini, ingawa imejitenga kutokana na milima mikubwa. 

Ardhi ya Lesotho haitumiki kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya kilimo, hivyo wakazi wake hupata changamoto ya uhaba wa chakula, huku wakitegemea zaidi mapato yatokanayo na kazi katika taifa jirani la Afrika Kusini. 

Kwa miongo mingi, maelfu ya wakazi wake hulazimika kuhamia Afrika Kusini kutafuta ajira, kutokana na uhaba wa fursa za kazi nchini mwao.

Watu wa Lesotho, ambao ni zaidi ya milioni mbili, wana baadhi ya kanuni za utamaduni na lugha zinazofanana na za Afrika Kusini. Lugha yao ya Sesotho, ni mojawapo ya lugha rasmi 11 za Afrika Kusini inayotajwa kuwa na idadi kubwa ya wazungumzaji wa Sesotho. Idadi hiyo milioni 4.6 ni zaidi ya mara mbili na nusu ya wakazi wa Lesotho.

Utajiri wa 'dhahabu nyeupe':

Rasilimali katika Lesotho ni chache, kutokana na kutawaliwa na milima ambayo ina mazingira magumu kwa kilimo kwenye maeneo ya chini.

Maji hayo ndiyo maarufu kama ‘dhahabu nyeupe,’ inauzwa nchini Afrika Kusini. Pia kuna almasi ambayo ni miongoni mwa bidhaa muhimu ambayo huuzia mataifa ya nje.

Kivutio cha kuteleza utelezi wa theluji: Wachezaji wa kuteleza kwa theluji kote duniani husafiri hadi Lesotho katika eneo la Afriski kushindana.

Eneo la kwanza la kufanyia mchezo huo huwa ni Kaskazini mwa Marekani au kwenye mteremko wa theluji Ulaya.

Lakini huko Lesotho, inajinadi zaidi katika michezo ya kuteleza kwa theluji, kwa sababu ya kuwa na eneo kubwa. 

Eneo hilo la Afriski lililoko mita 3,222 juu ya usawa wa bahari, imekuwa kivutio cha wageni kutoka Afrika na maeneo mengine duniani. 

Idadi kubwa ya maambukizi Ukimwi: Lesotho ina changamoto kubwa ya mambukizi ya juu ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Wastani uliopo ni takribani mmoja kati ya watano wazima wanaishi na VVU na maambukizi ni ya juu zaidi kuliko nchi nyingine Afrika, wakiwamo majirani, Namibia, Botswana na Eswatini. 

Urafiki mkubwa na Uingereza inayoisaidia Lesotho: Inaelezwa kwamba, kuna urafiki wa karibu Mwanamfalme Seeiso- ndugu mdogo wa Mfalme Letsie III na mwanamfalme Harry wa Uingereza.

Wawili hao walianzisha shirika la Sentebale linalofanya kazi na vijana walioathirika na HIV katika jamii za Lesotho.

Kiwango cha juu cha wanaojiua duniani: Mbali na athari za Ukimwi, pia Shirika la Afya Duniani (WHO) linataja asilimia 87.5 ya watu 100,0000 wanaopatwa na madhila Lesotho, hujiua kila mwaka.

Takwimu hiyo inatajwa kuwa ni kubwa mara 10 zaidi ya wastani wa dunia, hali inayoleta ugumu kutambua sababu kwa wengi wana hoja zaidi ya moja.

Wataalamu wanasema kuwa matumizi ya dawa za kulevya na pombe, ukosefu wa ajira na upungufu wa huduma za afya ya akili, ni baadhi ya sababu zinazochangia ongezeko hilo la kujiua.

MAISHA JAMII 

Wenyeji wa Lesotho wanajulikana kama Basotho: Baadhi ya bidhaa zao za kitamaduni ni mablanketi mazito na kofia zinazoendana na maarufu kwa jina ‘mokorotlo.’.

Kofia hizo hutumika kama nembo ya kitaifa na inaonekana katikati ya bendera yao Lesotho.

Blanketi hizo za Basotho, hutengenezwa kwa sufi nzito na zimejaa michoro ya kipekee yenye mvuto, kila moja ikielezea historia ya jamii yao.

Mablanketi hayo huvaliwa kwenye matukio maalum, pia wenyeji huwapatia wageni wao kama zawadi.

Kibiashara, wanauza sana vitambaa vya aina ya jinzi (jeans), Marekani: Ni aina ya kitambaa kigumu cha pamba kikihusishwa zaidi na soko la Marekani.

Viwanda vya nchi hiyo ndio vinatengeneza mavazi hayo, vimeunda jinzi kwa ajili ya chapa maarufu za Marekani kama vile Levi's na Wrangler.

Mwaka jana, Lesotho iliuza vitambaa na nguo zenye thamani ya dola milioni 237 (Sh. Trilioni 637.530) huko Marekani kupitia Sheria ya Ukuzaji na Fursa ya Afrika (AGOA), ambayo mauzo yake hayatozwi ushuru nchini Amerika.

Hivyo, nguo hizo zimeingia katika bidhaa za thamani zilizouzwa nchini Marekani kupitia mpango huo. Hata hivyo, viwanda vingi wanunuzi wake vinamilikiwa na Wachina na raia wa Taiwan walioko Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa kimataifa