VIWANGO vya joto duniani, hadi sasa, vinatajwa kuongezeka kila uchao. Shughuli za kibinadamu zinatajwa kuwa na mchango mkubwa katika hilo.
Shughuli za viwanda hasa kwa nchi zilizoendelea kama Marekani na China, zinatajwa kuongeza viwango vya mabadiliko ya tabianchi.
Ni siku chache zimepita kumetajwa, nchini Sudan Kusini, shule zote zimefungwa kwa muda wa wiki mbili, kutokana na joto kali.
Waziri wa Mazingira nchini humo, Josephine Napon, akatangaza hilo na kwamba, shule zitafungwa hadi hali itakapokaa sawa.
Inaelezwa kuwa tangu Februari mwaka huu, nchi hiyo inashuhudia joto kali, kukitajwa shule za msingi na sekondari zinazosemekana watoto walizimia.
Na kwamba, ushauri kwa umma ni kukwepa jua, kufanya kazi chini ya kivuli cha mti, kuvaa nguo za hariri, kunywa maji na kuepuka vinywaji vya kafeni.
Mwaka juzi - 2023, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa (WMO), lilithibitisha rasmi kuwa mwaka huo ndio mwaka wa joto zaidi katika rekodi za joto duniani.
Wastani wa hali ya joto ya kila mwaka duniani ikikaribia nyuzi joto 1.5, zaidi ya viwango vya kabla ya viwanda.
Makubaliano ya jijini Paris, Ufaransa wa Desemba mwaka 2015 kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanakabiliwa, yanalenga kupunguza ongezeko la joto la muda mrefu duniani.
Taasisi sita za kimataifa zilizotumika kuchunguza hali ya joto duniani na kuunganishwa na WMO, zinaonyesha kuwa wastani wa joto duniani ulikuwa juu kwa nyuzi joto 0.12 za sentigrdi.
Hiyo ni juu katika kulinganisha, kabla ya viwanda zama za miaka ya 1850 hadi miaka ya -1900. Hiy oni kwa vipimo vya mwaka wa 2023.
Halijoto duniani katika kila mwezi kati ya Juni na Desemba, iliweka rekodi mpya kila mwezi. Mnamo Julai na Agosti, ilikuwa miezi miwili ya joto zaidi kwenye rekodi.
Profesa Celeste Saulo wa nchini Argentina, ambaye ni Katibu Mkuu wa WMO anasema kuwa: “Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa ambayo binadamu anakabiliana nayo. Inatuathiri sisi sote, hasa walio hatarini zaidi.”
“Hatuwezi kumudu kusubiri tena. Tayari tunatenda, lakini lazima tufanye zaidi, na tunapaswa kufanya haraka.
“Ni lazima tupunguze kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa chafuzi na kuharakisha mpito hadi vyanzo vya nishati mbadala.
“Mabadiliko kutoka kwa baridi ya La Niña hadi joto la El Niño katikati ya 2023 yanaonyeshwa wazi katika ongezeko la joto kutoka mwaka jana.
“Ikizingatiwa kuwa el nino kwa kawaida huwa na athari kubwa zaidi kwa halijoto duniani baada ya kufika kilele, mwaka wa 2024 unaweza kuwa wa joto zaidi”.
Kumrejea Prof. Saulo, wakati matukio ya mvua el Niño yakatokea kuwa kawaida na kuja na kupita kutoka mwaka mmoja hadi mwingine.
Mabadiliko ya tabiachi ya muda mrefu, yanaongezeka ni kwa sababu ya shughuli za kibinadamu. Janga la tabianchi linazidisha janga la ukosefu wa usawa.
Unaathiri nyanja zote za maendeleo endelevu na kudhoofisha juhudi za kukabiliana na umaskini, njaa, afya mbaya, kuhama makazi na uharibifu wa mazingira na miaka tisa iliyopita imekuwa joto zaidi katika rekodi.
Ni mabadiliko ya tabianchi yameongeza hatari ya hali ya hewa kavu ya joto ambao inachangia kuchochea moto wa nyika, matendo ya binadamu yanaiteketeza dunia
KATIBU MKUU UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, katika taarifa yake anasema kwamba: "Vitendo vya binadamu vinaiteketeza dunia.
“Mwaka wa 2023 ulikuwa hakikisho tu la siku zijazo mbaya ambazo zinangoja ikiwa hatutachukua hatua sasa.”
Msomi Profesa Saulo anataja, ni lazima tujibu ongezeko la joto linalovunja rekodi kwa hatua ya kuvunja njia. Bado tunaweza kuepuka janga baya zaidi la tabianchi.
“Lakini tu, ikiwa tutachukua hatua sasa kwa nia inayohitajika kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5 na kutoa haki ya hali ya hewa.”
Profesa Saulo anahitimisha kuwa, ufuatiliaji wa muda mrefu wa hali ya joto duniani, ni kiashiria kimoja tu cha hali ya hewa na jinsi inavyobadilika.
Viashiria vingine anavitaja kuwa pamoja na viwango vya gesi chafuzi ya hewa, joto la bahari na uasidi, kiwango cha bahari, kiwango cha barafu ya bahari na usawa wa wingi wa barafu.
“Mabadiliko haya ya muda mrefu katika hali ya hewa yetu hupitia hali ya hewa yetu kila siku. Mnamo 2023, joto kali liliathiri afya na kusaidia kuchoma moto nyikani."
Mvua kubwa, mafuriko, vimbunga vya kitropiki vinavyoongezeka kwa kasi viliacha njia ya uharibifu, vifo, na hasara kubwa za kiuchumi.
MKATABA WA PARIS
Makubaliano ya Paris yanalenga kushikilia ongezeko la wastani wa halijoto duniani hadi chini ya 2°C juu ya viwango vya kabla ya viwanda huku ikifuatilia juhudi za kupunguza ongezeko la joto hadi 1.5°C juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda.
Jopo la serikali duniani vilivyojadili mabadiliko ya tabianchi, linasema kwamba hatari zinazohusiana na hali ya hewa kwa mifumo ya asili na ya binadamu ni kubwa zaidi kwa ongezeko la joto duniani kwa nyuzijoto 1.5 °C kuliko ilivyo sasa, lakini chini ya nyuzijoto mbili.
Utafiti uliofanywa na WMO na Ofisi ya MET ya Uingereza mwaka jana, ulitabiri kwamba kuna uwezekano wa asilimia 66 kwamba wastani wa joto la dunia karibu na uso wa dunia kati ya 2023 na 2027 utakuwa zaidi asilimia 1.5, juu ya viwango vya kabla ya viwanda kwa angalau mwaka mmoja.
Hiyo haimaanishi kutazidi zaidi ila kiwango cha nyuzo 1.5 sentigredi kilichobainishwa katika Mkataba wa Paris, unaorejelea ongezeko la joto la muda mrefu kwa miaka mingi.
Nafasi ya kuzidi kwa muda nyuzi 1.5 sentigredi, katika zama hizo kuelekea mwaka 2015, wakati ilikuwa karibu na sifuri.
Kwa miaka kati ya 2017 na 2021, kunatajwa kulikuwapo na uwezekano wa asilimia 10 zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED