TUNAPOUWEKA msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu England (EPL), kwenye historia, tunaweza kutazama waliong’ara zaidi mwezi uliopita hasa wikendi ya mwisho ambayo ni kama iliamua wapi linakoelekea taji hilo.
Bila shaka matatizo yamewakatisha tamaa waliokuwa washindani kwenye mbio za ubingwa Arsenal msimu huu, lakini walikuwa na nafasi ya kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni hadi pointi tano kabla ya mchezo wao wa nyumbani dhidi ya West Ham United. Wakati Wekundu hao walikuwa wanakwenda kucheza na Manchester City, nafasi kubwa ilikuwa imetokea kwa 'Washikabunduki' hao.
Hata hivyo, badala ya kuhitimisha wikendi hiyo tukiwa na mbio kali mikononi mwetu, wengi sasa wanatarajia kikosi cha kocha Arne Slot ndio mabingwa waliochaguliwa.
Ushindi wa mabao 2-0 mjini Manchester, saa 24 baada ya Arsenal kuchapwa 1-0 na West Ham, ulimaanisha kuwa Liverpool wana mkono mmoja kwenye taji lao la pili la Ligi Kuu tangu mwaka 1990.
Sote tunajua ni nani alitengeneza show ya kibabe na hapa tunawangalia wachezaji sita waliong’ara zaidi ndani ya Februari, twende pamoja sasa...
6. Joao Pedro (Brighton)
Hakukuwa na matatizo kwa Brighton Jumamosi iliyopita wakivuka pwani ya kusini kuwatembelea wakazi wa Southampton, na kuwaacha pale St. Mary's kwa kichapo cha mabao 4-0.
Safu ya mbele ya Brighton yote iling’ara, lakini alikuwa Pedro, ambaye hajapata matokeo mazuri zaidi kwa mwaka 2025 hadi sasa na amezuiwa na jeraha, ambaye alikuwa na uchezaji wa kipekee zaidi.
Mbrazil huyo aliungana vema na Georginio Rutter katika kukosekana kwa Danny Welbeck, na wawili hao waliungana kwa bao la kwanza. Pedro alikuwa na onesho la kifahari. Safu ya ulinzi ya Saints ilishindwa kabisa walishindwa kabisa kumsumbua mshambuliaji huyo wa Brighton ambaye anarejea katika kiwango chake.
5. Aaron Wan-Bissaka (West Ham)
Iliigharimu West Ham pauni milioni 15 tu kumleta Wan-Bissaka Mashariki mwa London, na beki huyo wa zamani wa Manchester United amethibitisha kuwa mmoja wa usajili bora wa majira ya joto.
Katika kampeni ya kutisha kwa ajili ya 'Wagonganyundo', Wan-Bissaka ameibuka kama mwanga mkali. Pengine alikuwa mchezaji bora wa klabu chini ya kocha Julen Lopetegui, na beki huyo aliendelea kuonesha kiwango kizuri tangu Graham Potter achukue nafasi hiyo.
Mwingereza huyo alimtumia Wan-Bissaka kama beki wa pembeni dhidi ya Arsenal, na akatoa mchezo mzuri wa pande mbili uliojumuisha pasi ya bao pekee katika mchezo huo. Kwa muda mrefu beki huyo alikosolewa kwa uzembe wake wa kumiliki mpira, lakini Wan-Bissaka alicheza kwa uwazi akiwa na mpira.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ndiye aliyetoa krosi ya moja kwa Jarrod Bowen aliyefunga bao wakati West Ham wakiwasumbua vilivyo Washikabunduki hao wa Kaskazini mwa London.
4. Lewis Hall (Newcastle United)
Hakukuwa na utulivu kuhusu ushindi wa Newcastle United dhidi ya Nottingham Forest, huku 'Magpies' hao wakilazimika kung'ang'ania dakika za mwisho licha ya kuwa mbele kwa mabao 4-1.
Beki wa kushoto Hall alitoa mchango muhimu katika ushambuliaji jambo ambalo liliibua ufufuo wa Newcastle baada ya kurudi nyuma mapema. Baada ya kumchambua Lewis Miley kwenye eneo la hatari na kusawazisha, wenyeji walipata penalti baada ya mpira wa krosi wa Hall kunawa na Ola Aina.
3. Daniel Munoz (Crystal Palace)
Wakiifunga Everton iliyopo kwenye kiwango, Crystal Palace imekuwa mojawapo ya timu bora zaidi za Ligi Kuu England 2025.
Beki wa pembeni Munoz alicheza jukumu la chini sana katika mafanikio yao msimu uliopita, na Mcolombia huyo amegundua upya kiwango chake cha nguvu chini ya safu ya kulia ya Palace.
Munoz alicheza vema katika raundi zote katika ushindi wa 2-0 wa Palace katika uwanja wa Craven Cottage na kumalizia onesho lake kwa umaliziaji bora uliofanikisha ushindi wa timu yake.
2. Bryan Mbeumo (Brentford)
Bryan Mbeumo alikuwa ameandikisha mchango wa bao moja pekee katika mechi sita kabla ya Brentford kupepetana pake kwenye Uwanja wa King Power.
'Nyuki' hao walikabiliana na timu ya Leicester yenye nia ya kupeleka mchezo kwa wenyeji wao baada ya kuwapa udhibiti Arsenal wikendi iliyopita, lakini wageni, wakiongozwa na Mbeumo, walikuwa wajanja sana kusonga mbele.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Cameroon, alifanya kazi bora sana, na kuandikisha bao na kutoa asisti katika ushindi wa Brentford wa mabao 4-0 dhidi ya 'Mbweha' hao.
1. Mohamed Salah (Liverpool)
Mohamed Salah asiyeepukika akifunga na kusaidia katika ushindi wa Liverpool kwenye Uwanja wa Etihad.
Mmisri huyo alifungua ukurasa wa mabao kutokana na uchezaji wa kijanja sana na baadaye akamtengenezea Dominik Szoboszlai baada ya kazi nzuri chini ya ulinzi dhidi ya Josko Gvardiol.
Idadi ni ya kushangaza, lakini kiwango cha Salah dhidi ya mabingwa hao watetezi kilikuwa kikiashiria zaidi kwamba yeye ni mchezaji wa kiwango cha juu zaidi.
Liverpool walikuwa na matatizo wakati fulani, hasa katika kipindi cha pili, wakati wa kulinda bao lao, lakini Salah aliendesha kama kikosi cha mtu mmoja akiongoza safu ya 'Wekundu' hao.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED