CAF yamtunuku Dk Samia tuzo ya usimamizi bora sekta ya michezo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:33 AM Nov 20 2025
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Shiriko la Soka barani Afrika (CAF), limemtunuku Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tuzo ya heshima kutokana na mchango mkubwa kwenye maandalizi ya uenyeji wa michuano ya CHAN 2024.

Pamoja na Rais Samia, tuzo hiyo pia amekabidhiwa Rais wa Kenya, William Ruto na Uganda, Yoweri Museven, kwa kuwa mataifa hayo ndio yaliyokuwa mwenyeji wa CHAN.

Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika mjini Rabat nchini Morocco na tuzo ya Rais Samia imepokelewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

CAF imesema imekabidhi tuzo hizo kuthamini maandalizi bora yaliyofanywa na wakuu hao wa nchi, sambamba na kuimarisha miundombinu ya michezo.

Mataifa hayo pia, ndiyo yanayotarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa Bingwa Afrika (AFCON) mwaka 2027.