CHADEMA, CHAUMMA jukwaani pamoja

By Elizabeth Zaya , Nipashe Jumapili
Published at 06:02 PM Jul 27 2025
Lembrus Mchome, Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Mwanga
Picha: Elizabeth Zaya
Lembrus Mchome, Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Mwanga

KWA mara nyingine, vigogo wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamejitokeza kwenye jukwaa la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na kuzungumza.

Vigogo hao ni Lembrus Mchome, Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Mwanga na Sigrada Mligo, Mwenezi CHADEMA Taifa.

Sigrada Mligo, Mwenezi CHADEMA Taifa.
Mchome amesema: "Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wamekosea ni kutokushiriki kweny uchaguzi wa mwaka huu, tunaomba ninyi CHAUMMA  ambao mnashiriki uchaguzi mwaka huu mhakikishe mnapambana kukiondoa Chama Cha Mapinduzi(CCM), msikubaki kupiga kura na kwenda kulala nyumbani, lindeni kura."

Siasa siyo uadui, nimealikwa na rafiki yangu Moza Ally ambaye ndiye mlezi wa chama chake kwenye jimbo hili la Kinondoni na anatia nia, nilikuwa naye kwenye chama changu na nimefanya naye kazi kwa muda mrefu, hivyo nimeona nije nimuunge mkono."

Wamesimma na kuzungumza leo, Julai 27, 2025 kwenye mkutano maalum wa CHAUMMA, Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.

Sigrada amesema: "Ni hatari kuruhusu bunge liongozwe na wabunge wa chama kimoja na ni hatari nyingine zaidi kuruhusu halmashauri ziongozwe na chama kimoja, kati ya vitu ambavyo wananchi wanatakiwa kuvikataa ni pamoja na hilo."

Mtiania wa ubunge (CHAUMMA), Jimbo la Kinondoni, Moza Ally amesema: "CHAUMMA kikinipa ridhaa ya kugombea ibunge jimbo la Kinondoni, hakuna mgombea yeyote wa CCM atakayeniweza, na kwa hilo nina uhakika na ninatuma salam wajipange."

Moza Ally

"Nimepambania jimbo hili kwa miaka 10 nalijua vizuri, naufahamu vizuri msitu wa Kinondoni, nafahamu namna ya kufyeka msitu wake na wapi pa kuotea moto wake."

" Kuna mbunge  hapa amekuwa akiwabagua wananchi, anachagua wachache wa kuwasaidia na wengi anawatenga, sasa ninamtumia salamu, mimi (Moza) sauti ya wananchi nimekuja, ninamtumia salamu, ajipange, lazima aondoke safari hii."