EAGT yaliombea taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu

By Shufaa Lyimo , Nipashe Jumapili
Published at 04:11 PM Jul 27 2025
news
Picha Shufaa Lyimo
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la EAGT Christomoo Ngowi.

KANISA la EAGT lililopo Temeke Dar es Salaam limeandaa mkutano wa injili ambao umefanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, kwa lengo la kuliombea taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Christomoo Ngowi amesema anaamini kupitia maombi hayo watapatikana viongozi wazuri kwakuwa hakuna linaloshindikana mbele ya Mungu.  

Mchungaji Diana Dionizi ambaye pia ni muubiri Mkuu wa mkutano huo amesema uchaguzi utafanyika kwa imani kubwa na kuwaweka viongozi ambao wamepata kura kihalali. 

"Naamini uchaguzi utafanyika vizuri kupitia mkutano wetu tutazidi kuliombea taifa letu na tutapata wale ambao tunawahitaji," amesema Dionizi.

Mchungaji Diana Dionizi